Please use this identifier to cite or link to this item:
http://ir-library.mmust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/1971
Title: | Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria |
Authors: | Wekesa, Winnie Musailo Simiyu, Fred Wanjala Opande, Nilson Isaac |
Keywords: | Vipengele, Fasihi, simulizi, vinayoona, Hali, katika, Taaluma Sheria |
Issue Date: | 31-Aug-2020 |
Publisher: | East Afriacan Journal of Swahili Studies |
Abstract: | Utafiti ulilenga kubainisha vipengele maalum vya Fasihi Simulizi vinavyooana na hali katika taaluma ya Sheria. Utafiti uliegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano ya utafiti. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha michakato miwili ya uteuzi wa sampuli; ikiwa ni uteuzi sampuli kimaksudina kinasibu. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tulioyahudhuria.Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usailina uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeoya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana nahali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshajikesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizizinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughulimbalimbali. |
URI: | https//doi.org/10.37284/eajss.2.2.193 https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/193/141 http://ir-library.mmust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/1971 |
Appears in Collections: | Journal Articles |
Files in This Item:
File | Description | Size | Format | |
---|---|---|---|---|
Vipengele vya Fasihi simulizi vinayoona na Hali katika Taaluma ya Sheria.pdf | 202.37 kB | Adobe PDF | ![]() View/Open |
Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.