Show simple item record

dc.contributor.authorWekesa, Winnie Musailo
dc.contributor.authorSimiyu, Fred Wanjala
dc.contributor.authorOpande, Nilson Isaac
dc.date.accessioned2021-12-31T09:06:26Z
dc.date.available2021-12-31T09:06:26Z
dc.date.issued2020-08
dc.identifier.urihttps://editoncpublishing.org/ecpj/index.php/ECJKISW/article/view/176/134
dc.identifier.urihttp://ir-library.mmust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/1976
dc.description.abstractUtafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshajkesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherEdition Consortium publishingen_US
dc.subjectNafasi , Fasihi,Simulizi, Katika, Kuwasilisha, Ujumbe, Kisheria, Uendeshaji,Kesi, Kitamadunien_US
dc.titleNafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusuen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record