Show simple item record

dc.contributor.authorKibigo, Mary Lukamika
dc.date.accessioned2020-12-11T08:43:11Z
dc.date.available2020-12-11T08:43:11Z
dc.date.issued2020-11-12
dc.identifier.urihttp://r-library.mmust.ac.ke/123456789/1441
dc.description.abstractShughuli nyingi za kijamii hutumia lugha inayopata maana katika muktadha inamotumika.Hali hii imechochea kutaka kujua namna Waisukha wanavyotumia lugha kuendeleza ubabedume katika majigambo yanayoghaniwa kwenyesherehe za upiganishaji fahalikisemantiki.Utafiti huu ulichunguzaubabedume miongoni mwa Waisukha jinsi unavyodhihirika katika Majigambo yaMiviga yaShilembe naMchezasiliwa Mayo. Vipashiovya lugha vinavyosheheniubabedumekatika majigambo hayovilihakikiwakwamtazamo wa kisemantiki. Utafiti uliongozwa na madhumuni haya: kupambanuavipashiovya lugha hususannomino,vishazi na vitenzi katika majigambo ya miviga ya Shilembena MchezasiliwaMayo vinavyodhihirisha ubabedume miongoni mwa Waisukhakisemantiki, kuhakiki tamathali za usemi zinazosheheni ubabedumekwa mtazamo wa kisemantiki na kutaliinafasi ya lugha, historia na itikadi za Waisukha katika kujenganakudumisha ubadedume.Utafiti huuuliongozwa na nadharia mbili: Nadharia ya UCHAMAWADIna Uwezo-Uume.Wachangiaji mashuhuri katika nadharia ya UCHAMAWADIni wataalam kama vile; Gee(1990), Fairclough (1992), Teun Van Dijk (1993)na Wodak(2001). Iliwekewa msingi nakazi mbalimbaliza wataalam hawa. Hutambua uamilifu wa lugha katika jamii. Mihimili yake mikuu ni; uhakiki, uwezo au mamlaka, historia na itikadi. Nadharia ya Uwezo-Uume iliasisiwa na Robert Bly (Well & Holland, 2001) na kuendelezwana Connell (1995). Inahusisha mahusiano ya wanawake na wanaume katika jamii. Baadhi ya mihimili yake ni; itikadi za kijamii ambazo huongoza fikra, mitazamo na mielekeo ya wanajamii kuhusu hali mbalimbali za kijamii. Nadhariahizizilitumiwa ili kuchangiana. Utafiti huu ulifanywa katika Kaunti Ndogo yaShinyalu, Kaunti ya Kakamega. Watafitiwa walikuwa fanani na washiriki katika sherehe za Shilembena Mchezasiliwa Mayo.Usampulishaji ulifanywa kwa kutumia aina tatu.Utafiti ulilenga kukusanya majigambo ishirini na sabakimaksudi kutegemea nasaba ishirini na saba za Waisukha. Majigambo kumi na sita yalikusanywakwa kutumia uteuzi wa kimapokezano. Uteuzi wa kimaksudi ulitumiwa kuteua nasaba saba zilizo na majigambo maarufu na uteuzi wa kinasibu ukatumiwa kuchagua majigambo tisa. Jumla ya majigambo yaliyotumiwa yalikuwa kumi na sita. Mbinu za Uchunzaji-Shiriki na Kiethnografia zilitumiwa na zilijumuisha kuishi na watafitiwa, kushiriki, kushuhudiasherehe hizo pamojana kuwahoji ili kukusanya majigambohayo.Data iliwasilishwa na kuchanganuliwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano, picha navielelezo. Matokeo yamebainisha kuwa,lugha ni kipengele muhimu cha jamii ya Waisukha kwa vile humsawiri mwanamume Mwisukha kama aliye na mamlaka zaidi ya mwanamke. Hali hii itafaidi jinsia ya kike kwa vile wanaume watayashughulikia majukumu yao kikamilifu katika jamii. Utafiti umebainisha kuwa,uwezo wa mwanaume umetamalaki katika majigambo ya Waisukha yaliyosheheni vipashio vya lughakisemantiki. Unatarajiwa kuupanua uwanja wa Fasihi Simulizi na Isimu kwa kulikuza suala la kuchanganua majigambo, kipera ambacho ni muhimu katika Fasihi Simulizi kwa mtazamo wa kisemantiki. Utafiti unatoa mchango katika kuelewa umuhimu wa Shilembena Mchezasiliwa Mayona mila, desturi na itikadi za Waisukha zinazowasilishwa kutoka kizazikimoja hadi kingine kupitiamasimulizi ya Mwafrika.Utafiti huu unanuiakuwachochea wasomi wa Fasihi Simulizi na Isimu wa baadaye kuchanganuaFasihi Simulizi kwa kina zaidi kwa kuangazia vipashiovya lugha na kuzua mwingilianotaalumakatika Kiswahili.en_US
dc.description.sponsorshipMMUSTen_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherMMUSTen_US
dc.subjectUbabedume, Majigambo, Miviga, Shilembe, Mchezasili, Semantikien_US
dc.titleUBABEDUME KATIKA MAJIGAMBO YA MIVIGA YA SHILEMBE NA MCHEZASILI WAMAYOMIONGONI MWA WAISUKHA NCHINI KENYA KWA MTAZAMO WA KISEMANTIKIen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record