Vipengele vya Fasihi Simulizi Vinavyooana na Hali Katika Taaluma ya Sheria
Date
2020-08-31Author
Wekesa, Winnie Musailo
Simiyu, Fred Wanjala
Opande, Nilson Isaac
Metadata
Show full item recordAbstract
Utafiti ulilenga kubainisha vipengele maalum vya Fasihi Simulizi vinavyooana na hali katika taaluma ya Sheria. Utafiti uliegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano ya utafiti. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha michakato miwili ya uteuzi wa sampuli; ikiwa ni uteuzi sampuli kimaksudina kinasibu. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tulioyahudhuria.Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usailina uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeoya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana nahali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshajikesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizizinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughulimbalimbali.
URI
https//doi.org/10.37284/eajss.2.2.193https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/193/141
http://ir-library.mmust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/1971
Collections
- Journal Articles [374]