Show simple item record

dc.contributor.authorOKIYA, OUMA EDMOND
dc.date.accessioned2026-04-14T13:34:13Z
dc.date.available2026-04-14T13:34:13Z
dc.date.issued2025-11
dc.identifier.urihttps://ir-library.mmust.ac.ke/xmlui/handle/123456789/3345
dc.description.abstractLugha ya Kiswahili ina dhima muhimu katika jamii kwa hivyo changamoto zinazoikabili kwa vyovyote vile zinastahili kutatuliwa. Mojawapo ya changamoto hizi ni athari ya lugha ya kwanza kwa ujifunzaji wake. Hali hii huathiri wanafunzi kwenye viwango vyote vya elimu ikiwemo shule za msingi na hudhihirika kwa namna mbalimbali ikiwemo katika uandishi wa insha. Ukiukaji wa sheria za kisarufi za Kiswahili huchangia hali hii. Hivyo basi, Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza makosa ya kisarufi katika insha za wanafunzi wa shule za msingi katika mtaala mpya wa elimu ya umilisi katika Gatuzi dogo la Butula. Madhumuni yalikuwa; kubainisha makosa ya kisarufi katika insha za wanafunzi wa gredi ya sita wa Kiswahili wa mtaala wa elimu ya umilisi, kuchunguza chanzo cha makosa ya kisarufi katika insha za wanafunzi wa gredi ya sita wa Kiswahili wa mtaala wa elimu ya umilisi na kupendekeza mikakati ya kupunguza makosa ya kisarufi katika insha za wanafunzi. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Makosa (NUM) ambayo iliasisiwa na Corder (1967), ambaye anasema kuwa kufanya kosa ni njia mojawapo ya kujifundisha lugha ya pili. Kwa hivyo, mwanafunzi anapofanya kosa, asiadhibiwe bali chanzo cha kosa kibainishwe. Muundo wa utafiti ulikuwa wa usoroveya elezi. Eneo la utafiti lilikuwa gatuzi dogo la Butula. Kundi lengwa lilikuwa wanafunzi 1100 wa gredi ya sita pamoja na walimu 72 wa Kiswahili wa shule 72 za msingi za kutwa. Mbinu za ukusanyaji data zilikuwa: uchunzaji, hojaji, usaili na uchanganuzi nyaraka. Vifaa vya utafiti vilivyotumiwa vilikuwa hojaji, orodha ya uchunzaji, mwongozo wa usaili na mwongozo wa uchanganuzi nyaraka. Sampuli za kimaksudi, kitabakishi na nasibu zilitumika. Usampulishaji kimaksudi ulitumika kuchagua shule 22 za msingi za kutwa na walimu 22 wa kiswahili. Usampulishaji kitabakishi ulitumika kugawa shule katika makundi huku usampulishaji nasibu ukitumika kuchagua wanafunzi 330 walioshiriki kwenye utafiti. Data ilichanganuliwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo na uchanganuzi wa kiidadi. Kipengele cha uchanganuzi kilikuwa matini zenye makosa ya kisarufi. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo katika aya, majedwali na chati. Matokeo ya utafiti yalibaini makosa ya kisarufi katika insha za wanafunzi wa mtaala wa umilisi kama ya kifonolojia (ubadilishaji wa sauti, udondoshaji wa sauti, uchopekaji wa sauti, uyeyushaji). Makosa ya kimofolojia (kudondoa viambishi katika neno, kuunganisha na kutenganisha maneno visivyofaa). Makosa ya kisintaksia (upatanisho wa kisarufi katika sentensi). Makosa ya kisemantiki (matumizi ya msamiati usiofaa na mrundiko wa maneno katika sentensi). Chanzo cha makosa ya kisarufi yalitambuliwa kama: kutofahamu wakati wa kutumia sauti zingine, mielekeo ya wanafunzi, mbinu zisizofaa za ufundishaji miongoni mwa mengine. Matokeo yalionyesha kuwa makosa ya kisarufi yanaweza kutatuliwa kwa njia anuai kama: uhamasishaji wa wazazi kuhusu mfumo wa elimu ya umilisi, uandishi wa insha mara kwa mara, miongoni mwa mengine. Utafiti unahitimisha kuwa makosa ya kisarufi katika insha za wanafunzi wa Kiswahili katika mtaala wa elimu ya umilisi gatuzi dogo la Butula ni mengi na yanajumuisha makosa ya kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na kisemantiki. Ingawa makosa mengi yametokana na athari ya lugha ya kwanza mengine yametokana na vyanzo mbalimbali. Mikakati mwafaka ikitumika kukabili tatizo hili, wanafunzi wataweza kuepuka makosa mengi. Uhamasishaji wa wazazi kuhusu elimu ya umilisi ni mojayapo ya mikakati mwafaka ya kurekebisha makosa haya. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, makosa ya kisarufi yalijitokeza katika insha za wanafunzi kisha vyanzo vyake kuchunguzwa, Mapendekezo yalitolewa ili kupunguza makosa haya kama vile Wizara ya Elimu kufuatilia na kuchunguza namna mwalimu anafundisha. Utafiti huu utawafaa washikadau wa elimu kama vile wanafunzi, walimu pamoja na maafisa wa elimu ili kubuni sera zinazofaa kuimarisha ufunzaji wa Kiswahili.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherMMUSTen_US
dc.titleUCHANGANUZI WA MAKOSA YA KISARUFI KATIKA INSHA ZA WANAFUNZI WA GREDI YA SITA WA MTAALA WA UMILISI WA SHULE ZA MSINGI KATIKA GATUZI DOGO LA BUTULA BUSIAen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record